Makala: Urejeshwaji wa CSR katika miradi ya Gesi asilia na mafuta, je unazingatia mahitaji ya jamii husika?
25 May 2024, 11:13 am
Na Musa Mtepa
Tanzania imepitisha sheria inayowataka makampuni kutoa sehemu ya mapato yao kusaidia jamii wanakofanya biashara au uzalishaji. Makampuni haya yanatakiwa kuchangia wastani wa 0.7% ya mapato yao kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya jamii husika. Michango hii inajulikana kama Corporate Social Responsibility (CSR), ambayo inasaidia serikali katika kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayozunguka mradi husika.
Karibu kwenye makala haya ambapo leo tunaangazia, “UREJESHWAJI WA CSR KATIKA MIRADI YA GESI ASILIA NA MAFUTA NCHINI: JE, UNAZINGATIA MAHITAJI YA JAMII HUSIKA?”
Kupitia makala haya, utasikia maoni ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Msimabti, Mngoji, na Msakala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, na Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Petroli ya Upstream Tanzania (PURA).
Mwandishi na msimulizi wa makala haya ni mimi, Musa Mtepa wa Jamii FM Radio.