Jamii FM

Nini kifanyike kuondoa unyanyapaa wa walemavu katika jamii?

24 December 2024, 12:31 pm

Ujumbe unaoonyesha kuwa unyanyapaa ni kosa kisheria. Picha na mwandishi wetu

Na Grace Hamisi

Unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu ni changamoto inayowakumba katika sehemu mbalimbali za maisha yao. Mara nyingi, watu wenye ulemavu huonekana kana kwamba hawana uwezo wa kujitetea au kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii. Katika makala hii, tunachunguza hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuondoa unyanyapaa huu na kuleta usawa kwa wote.

Tutapata maoni kutoka kwa wanajamii ambao ni wadau muhimu katika kupunguza unyanyapaa na kutetea haki za watu wenye ulemavu.

Shazili Salehe mkazi wa Newala mkoa wa Mtwara, anasisitiza umuhimu wa ushirikishaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli zinazofanywa na wale wasio na ulemavu. Anaamini kuwa hili ni hatua muhimu katika kujenga jamii jumuishi.

Kwa upande wake, Sadiki Chivalamba mkazi wa kijiji cha Kitangali, anapendekeza elimu kwa jamii kuhusu usawa wa watu wenye ulemavu na wengine elimu hii. Anasema ni msingi wa kuondoa mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu.

Naye Neema Jerome, Mkurugenzi wa Newala Youth Organization (NEYO), asasi isiyo ya kiserikali inayofanya kazi wilayani Newala, anaeleza kuwa kushirikisha watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za kijamii kutasaidia kupunguza unyanyapaa na kuongeza usawa wa kijamii.

Jiunge nami katika makala hii tunapojadili kwa kina jinsi ya kujenga jamii jumuishi isiyo na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu.