Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ataka mkoa ufikie afua ya lishe ya kitaifa
24 February 2022, 12:37 pm
Na Gregory Millanzi
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wadau wa lishe katika mkoa huo kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao ili kufikia viwango vilivyowekwa kitaifa katika usimamizi wa afua za lishe.
Gaguti amesema hayo kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa usimamizi wa afua za lishe kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2021, na kusema Halmashauri itakayofanya vibaya katika afua za lishe haitaruhusiwa kuingia kwenye kikao na badala yake wahusika watachukuliwa hatua.
Kwa upande wake afisa lishe Mkoa wa Mtwara Herieth Kipuyo amewataka maafisa lishe kwenye kila halmashauri kuongeza uwajibikaji katika kufanya kazi ili kupunguza utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano katika maeneo yao.
Mkoa wa Mtwara katika kipindi cha mwaka 2021 ulishika nafasi ya tatu kitaifa katika suala la lishe na kwamba mkuu wa mkoa huo amewataka wadau wa lishe hasa maafisa lishe kufanya kazi kwa bidii ili kusalia katika nafasi ya tatu ya mwaka jana au kupanda hadi kufika nafasi ya kwanza kitaifa.