Viongozi wa Dini wasisititwa kupiga vita tabia chafu
22 March 2023, 12:38 pm
Watanzania hawana tabia ya ndoa za jinsia moja hivyo tamaduni za nje zisiruhusiwe kuingia nchini huku akiwataka jamii kupiga vita madangulo yote yanayofanya biashara ya ngono
Na Musa Mtepa
Jamii na Viongozi wa Dini wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita tabia chafu ambayo haipo katika mila na Desturi ya kitanzania .
Akizungumza na Mashekhe waliojitokeza kwenye Dua ya kumuombea Rais wa jamhuri ya muungano wa Dr Samia Suluhu Hassani kutimiza miaka miwili madarakani viwanja vya mashujaa Manispaa ya Mtwara Mikindani, mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Mtwara Saidi Musa Nyengedi amesema kuwa Watanzania hawana tabia ya ndoa za jinsia moja hivyo tamaduni za nje zisiruhusiwe kuingia nchini huku akiwataka jamii kupiga vita madangulo yote yanayofanya biashara ya ngono.
Aidha Mwenyekiti amesema kuwa mmomonyoko wa maadili ni mkubwa hivi sasa mataifa ya nje yanataka kuharibu mila na Desturi za kiafrika hivyo viongozi wa Dini ,Wazee akina Baba na mama wawe mstari wa mbele kupiga vita tabia hizo chafu.
Kwa upande wa viongozi wa Dini Mkoani Mtwara wameitaka jamii wasiwe tayari kukubali kuingiliwa na mambo yasiyostahili katika mila na desturi za nchi huku wakipinga kuwa hakuna Dini inayotoa haki kwa mapenzi ya jinsia moja.