Ushiriki wa mwanamke kwenye nafasi za uongozi
20 November 2023, 11:12 am
Nimefarijika kuona jinsi gani wananchi wa Mkunwa na viongozi wao wapo tayari kuhakikisha kwamba wanawake wenye uwezo na vigezo wanaweza kushiriki katika nafasi mbalimbali za uamuzi.
Na Musa Mtepa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefurahishwa na Maendeleo ya Mradi wa ‘’Mwanamke Ongoza “ unaotekelezwa katika kata ya Mkunwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wenye lengo la kumuelimisha na kuhamasisha Mwanamke kuingia kwenye nafasi za uongozi na uamuzi.
Akizungumza na Jamii fm Radio Mratibu wa Mradi huo Bi Zainabu Mmary amefarijika kuona jinsi gani wananchi wa Mkunwa na Viongozi wao wapo tayari kuhakikisha kwamba Wanawake wenye uwezo na vigezo Wanaweza kushiriki katika nafasi mbalimbali za uamuzi.
Nae Coletha Chiponde katibu wa kituo cha taarifa na Maarifa kutoka katika kijiji cha Mkunwa ameelezea jinsi gani wanavyo toa Elimu juu ya ukatili wa kijinsia na uhamasishaji wa Wanawake kushiriki katika kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi na uamuzi.
Sambamba na hilo baadhi ya Wanawake kutoka kata ya Mkunwa wameelezea changamoto zinazo wakwamisha kushiriki na kupigania nafasi mbalimbali za uongozi na uamuzi huku wakizishukuru asasi za kiraia zinazoendelea kutoa Elimu juu ya ushiriki wa Mwanamke katika nafasi za uongozi.
Nao baadhi ya Wanaume kutoka vijiji vya Nanyati na Kawawa wamewataka Wanaume kubadilika na kuwapa nafasi Wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi huku wakielezea kuwa mwanamke akiwa kiongozi anakuwa Mwadilifu katika nafasi yake.