

20 May 2021, 19:12 pm
Na Karim Faida
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewaomba wananchi wa Mtwara kumpa ushirikiano zaidi ya ule alioupata aliyekuwa mkuu wa mkoa huu Ndugu Gelasius Byakanwa.
Amesema hayo leo katika ukumbi wa Boma uliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mtwara mbele ya watumishi mbalimbali wa serikali wa mkoa huu pamoja na waandishi wa habari.
Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa huu Ndugu Gelasius Byakanwa, amempongeza mkuu wa mkoa huyo mpya kwa kuteuliwa tena huku akimuomba kulisimamia swala la zao la korosho pamoja na rasilimali za Gesi na Mafuta.