Wanafunzi wa Mtwara vijijini waomba kupewa fedha za taulo za kike
19 October 2020, 11:10 am
Baadhi ya Wanafunzi wa kike mkoani mtwara wamewataka wazazi kutenga bajeti kwa ajili kununua taulo za kike, ikiwa ni moja ya njia ya kutokomeza mimba za utotoni.
Wakizungumza na jamii fm radio wanafunzi hao wamesema kuwa ukosefu wa taulo za kike (PEDI) unawapelekea wasichana waliobado shuleni kutojikita kwenye masomo, na kushiriki ngono kwa ajili ya kupata pesa, ili kukidhi hitaji hilo muhimu ambalo kwenye familia nyingi hususan Mtwara halipewi kipaumbele.
Kwa upande wa baadhi ya wazazi wamesema kuwa mbali na kutimiza hitaji hilo ,wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto wao juu ya masuala ya ukuaji na mabadiliko ya mwili,ili kuwaepusha na vishawishi ambavyo vitawapelekea kupata ujauzito katika umri mdogo.
Aidha Jamii fm imezungumza na Daktari katika hospitali ya rufaa ya mkoa Ligula mkoani Mtwara Deogratius Makoti,ambapo amesema kuwa kupata mimba katika umri mdogo kunaweaza kusababisha mama kupata madhara wakati wa kujifungua ikiwemo kupata fistula.
Hata hivyo kwa mujibu wa Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Isack Bilali amesema kuwa kwa mwaka 2019 wanafunzi wawili wa shule za msingi na wengine wanane wa sekondari wamepata mimba wakiwa shuleni.