Jamii FM
Sijasoma ila nawasaidia wazazi
19 April 2021, 12:01 pm
Na karim Faida
Nchi ya Tanzania imebarikiwa vyanzo vingi vya maji ambavyo pia vinatumika katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na shughuli za uvuvi ambazo zinasaidia kuingiza kipato kwa watu wanaoishi jirani na chanzo fulani cha maji mfano bahari, Maziwa, mito hata mabwawa.
Michael Hashim ni mtoto wa miaka 16 mkazi wa mtaa wa sokoni kata ya Mtawanya manispaa ya Mtwara mikindani mkoani hapa ambae hakubahatika kwenda shule anasema anatumia fursa ya uwepo wa mto Liyakaya uliopo Jirani na mtaa wake kuvua samaki na kuwauza.
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mto huo umefurika na maji mengi yanaelekea baharini kupitia Kwenye njia maalumu ambayo Michael na wenzake wanaenda kuwatega samaki hao.
Michael amekuwa akiwasaidia wazazi wake kwa kuwa akipata samaki hao baadhi anawauza ili kupata pesa ya kununua unga na wengine huwabakisha kama kitoweo.
Hata hivyo Michael anasema anapenda kufanya kazi hiyo kwa kuwa inampa pesa ya matumizi na pia ni kama sehemu ya kucheza kwake.