Athari ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri upatikanaji wa samaki
19 March 2024, 15:55 pm
“Ongezeko la joto Baharini na uwingi wa maji ya mvua kutoka Kwenye mito mbalimbali kumechangia kwa kiasi kikubwa kupungua upatikanaji wa Samaki “
Na Musa Mtepa
Baadhi ya Wavuvi wa wanaofanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari na Pwani ya Mkoa wa Mtwara wameelezea changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi inavyo waathiri katika upatikanaji wa Samaki na hali yao ya kiuchumi.
Wakizungumza na Jamii Fm Radio March 18,2024 Wavuvi hao wamesema kuwa ongezeko la joto Baharini na uwingi wa maji ya mvua kutoka Kwenye mito mbalimbali kumechangia kwa kiasi kikubwa kupungua upatikanaji wa Samaki .
Saidi Dadi ni mkazi wa mtaa wa Magomeni Manispaa ya Mtwara ambae pia ni mvuvi samaki kwa zaidi ya miaka 30 amesema zamani Samaki walikuwa hawapatikani umbali mrefu ukilinganisha na sasa hivi ambapo huwalazimu kwenda umbali mrefu kuwapata.
Naye Sheha Shante Mwenyekiti wa Wavuvi Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema kutokana na upatikanji wa kuwa mchache imepelekea maisha ya Wavuvi kuwa magumu kiuchumi huku akiiomba serikali kuwaangali kwa jicho la kwa kuwapatia mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtandao Wilaya utunzaji wa Mazingira ya Pwani na Bahari (BMU) Shabani Mayonzi amesema ili kurejesha katika hali yake ya asili ya Bahari lazima Serikali na Wadau mbalimbali kuwekeza katika utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira ya Bahari ikiwemo upandaji wa mikoko pamoja na ulimaji wa zao la Mwani.