Jamii FM

KIPINDI – Utekelezaji wa ahadi za kwenye Kampeni 2024

18 April 2025, 18:06 pm

Mwanamke akiwa katika mwonekano wa eneo linalosadikika anaishi Rukia Mnyachi. picha kwa msaada wa AI

Katika kuonyesha hamasa na mafanikio ya wanawake vijijini katika kushiriki uongozi wa serikali za mitaa, kwa kuangazia ushindi wa Rukia Mnyachi kama Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi, aliyehamasishwa na kituo cha taarifa na maarifa kinachojishughulisha na masuala ya kijinsia, na jinsi alivyoleta suluhisho la haraka kwa changamoto ya maji kijijini kwao

Imeandaliwa na Musa Mtepa, Mwanahamisi Chikambu na Gregory Millanzi

Wanawake waishio vijijini wanazidi kuonyesha uwezo na uthubutu katika uongozi, na ushahidi wa wazi ni ushindi wa Rukia Mnyachi, Mwenyekiti mpya wa Kijiji cha Nyengedi, aliyechaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji uliofanyika Novemba 2024.

Katika mahojiano maalumu, Bi. Rukia amefunguka kuhusu safari yake ya kiuongozi, akieleza kuwa alihamasishwa na Coletha Chiponde ambaye ni Mratibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Halmashauri ya Wilaya ya Mkunwa, ambacho kinalenga kuwawezesha wanawake na kushughulikia masuala ya kijinsia.

Kipindi hiki kinamulika si tu ushindi wake, bali pia mafanikio yake ya haraka katika kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika Kijiji cha Nyengedi. Kupitia jitihada na uongozi wake madhubuti, wakazi wa Nyengedi sasa wanapata huduma ya maji kwa urahisi zaidi, jambo lililowaletea matumaini na faraja.

Ushindi na mafanikio ya Rukia ni kielelezo cha mabadiliko chanya katika ushiriki wa wanawake kwenye uongozi, hasa maeneo ya vijijini. Ni wito kwa jamii kuendelea kuwaunga mkono wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi.

Kusikiliza kipindi hiki, Bonyeza Hapa