TPA yatakiwa kuitafutia masoko Bandari ya Mtwara
18 February 2023, 19:09 pm
Na Musa Mtepa
Naibu katibu mkuu wizara ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dk Ally Possi ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kushirikiana na Serikali kutafuta masoko ya kuiwezesha Bandari ya Mtwara kufanya kazi kikamilifu kutokana na uwekezaji uliopo hivi sasa katika Bandari hiyo.
“Serikali imewekeza katika Bandari ya Mtwara kwenye ujenzi wa Gate na miundombinu mbalimbali hivyo ni wakati kwa mamalaka ya Bandari kuhakikisha inapanua masoko kwa kuwavutia wafanya biashara kutola Comoro, Zanzibari na nchi jirani kutumia Bandari hiyo.”
Mhe. Dk Possi ameyasema hayo jana Februari 17, 2023 alipofanya ziara katika Bandari hiyo yenye lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo.
Serikali imewekeza katika Bandari ya Mtwara kwenye ujenzi wa Gate na miundombinu mbalimbali hivyo ni wakati kwa mamalaka ya Bandari kuhakikisha inapanua masoko kwa kuwavutia wafanya biashara kutola Comoro, Zanzibari na nchi jirani kutumia Bandari hiyo.
Sambamba na hilo Mhe. Dk Possi amesema kuwa Wizara ya Ujenzi na Sekta ya Uchukuzi inalengo makubwa ya kufungua ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor) pamoja na kuangalia Bandari ya Mtwara katika kuipa ahueni Bandari ya Dar es salaam .
Akizungumzia hali ya utendaji kazi Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Ndg. Norbert Kalembwe amesema kuwa kumekuwa na mwendelezo mzuri katika makaa ya mawe na meli za mara kwa mara zinazobeba makaa hayo huku wastani wa tani Milioni 1.3 kwa kipindi cha miezi 7 iliyopita huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa asilimia 150% ukilinganisha na malengo waliyo jiwekea ikiwa ni tani laki 4.2 kwa kipindi cha mwaka mzima .