Mahitaji ya kupata habari ni makubwa kwa sasa – Said Swallah
13 February 2024, 11:30 am
Na Grace Hamisi, Amua Rushita
Kila ifikapo Februari 13 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya Redio Duniani ambapo huzungumziwa mchango wa redio katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo, changamoto wanazokutanazo jamii na kuziwasilisha kwa wenye mamlaka .
Lakini pia redio imekuwa ikitengeneza urafiki na umoja baina ya watu katika jamii, katika kuelekea maadhimisho hayo Jamii FM Radio imepata nafasi ya kuzungumza na mkurugenzi mtendaji wa Jamii FM Ndugu Said Swallah ambapo ameelezea umuhimu wa redio pamoja na sababu za kuanzishwa kwa kituo hiki cha habari kwa mkoa wa Mtwara.
Swallah amesema “Kinachotolewa redioni kinagusa makundi mbalimbali, kasi imeongezeka ya uanzishwaji wa redio na pia maudhui yamekuwa na mabadiliko makubwa, kinachojitokeza ni kuwa mahitaji ya kupata habari ni makubwa kwa sasa na hii imetokana na dunia kuwa kijiji”
“Mtu anaweza kuwa kijijini lakini akawa anafuatilia habari za mataifa mengine yaliyo nje ya eneo lake”. ameongezea Swallah
Karibu usikilize mahojiano haya juu ya siku ya redio duniani