Ngedere na Tumbili wavuruga shughuli za kilimo
11 February 2022, 11:53 am
Wanyama pori (Tumbili na Ngedere) wamekuwa kikwazo kwa wananchi kufanya shughuli za kilimo kwa ufasaha kwa baadhi ya kata za Halmashauri ya Mtwara vijijini hali inayopekea kukatamaa na shughuli hizo.
Akichangia Taarifa ya kamati ya uchumi ,ujenzi na Mazingira Diwani wa Kata ya Ndumbwe Mh Abdully Mahupa kwenye kikao cha Madiwani kilichofanyika Februari 8, 2022 kwenye ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Mustafa Sabodo ameiomba kamati hiyo kutengeneza njia mzuri ya kuwasaidia wananchi kuwazuia wanyama hao.
Akizitaja kata zinazo athiriwa na wanyama hao kuwa ni pamoja na Kata ya Ndumbwe, kata ya muungano,Mpapura na kata ya Libobe .
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Maisha Mtipa amesema kuwa wao kama Halmashauri watazungumza na wataalamu wa wanyamapori ili kutembelea kata hizo waweze kuona namna ya kuwadhibiti wanyama hao.