Wananchi hameni
8 April 2021, 19:35 pm
Wananchi waishio Kando ya bwawa la Kijiji Cha Msakala, kata ya Ziwani Mtwara Vijijini Jana Tarehe 07 Aprili, 2021 wametakiwa kuondoka mara Moja kuepuka kadhia ya kuharibiwa Makazi yao pindi bwawa linapojaa.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan D. Kyobya alipotembelea bwawa lililojaa Maji Kisha kuvuka Kingo na kuharibu Miundombinu ya Barabara, Nyumba na Vyoo.
Kwa mujibu wa taarifa za Mwenyekiti wa Kijiji cha Msakala Bwn. Ismail Liyaya amesema kuwa zaidi ya Nyumba 17 zimebomoka hivyo kufanya Kaya nyingi kukosa Makazi.
Ameendelea kusema kuwa bwawa hilo lenye zaidi ya Miaka 46 lilichimbwa kwa minajili ya kutumika kwa Shughuli za kibinadamu ambapo halikuwahi kufurika Kama ilivyotokea kwa Sasa.
Kutokana na Hilo Wananchi wengi wakawa wanajenga Makazi kwa kulifuata bwawa hilo na kusababisha Makazi kuongezeka Jambo ambalo ni kinyume na utaratibu hivyo kutakiwa kuhama Mara baada ya kupewa notisi.
Kutokana na madhara yaliyojitokeza hivi karibuni imeagizwa Wananchi hao kuhama maramoja huku taratibu zingine za kufanya marekebisho kitaalamu yakiendelea.
Source: Isaac Bilali