Makala: Matumizi bora ya gesi ya kupikia majumbani
5 August 2023, 14:58 pm
Na Musa Mtepa
Makala haya yanasimulia matumizi bora ya nishati ya kupikia majumbani maarufu kama gesi ya kupikia, ambapo mkoani Mtwara tayari wananchi wanatumia mitungi ya kampuni mbalimbali za gesi kwa ajili ya kupikia pia tayari kuna mtandao wa gesi kwa nyumba zilizounganishwa kwa ajili ya kupikia kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Waliosikika katika makala haya ni Omari Leba ambaye ni muuzaji na wakala wa mitungi ya Gesi majumbani, mwingine ni Ismail Chivalavala ambayeni mwananchi na mtumiaji wa huduma hii ya Gesi anayeishi Mtaa wa chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani pamoja na Ispekta Ambros Ndunguru kutoka jeshi la zima moto na uokoaji mkoani mtwara ambao wote kwa pamoja wamefanikisha kutoa elimu katika makala haya.