Halmashauri kuu CCM Newala watoa azimio la kero ya Maji kwa serikali
3 December 2021, 15:51 pm
“Baada ya kuona Hali ya Maji Wilaya ya Newala inaporomoka poromoka kila mwaka, na wakati mwingine wakati Nagombea Ubunge Maji huwa yanapatikana kwa asilimia 60, Wabunge wote wa Mtwara tulikubaliana kuonana na Waziri wa Maji na tukampa kilio chetu, Waziri wa Maji akamtuma Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na tukakagua Mradi wa maji Mitema na tukakuta maji yanamwagika na umeme unafanya kazi “
Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum – Mh. George Mkuchika
Na Gregory Millanzi, Mtwara
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Newala, wametoa tamko la kuiomba serikali kumaliza tatizo la Maji katika Wilaya hiyo, ambayo kwa sasa maji yanauzwa kwa ndoo moja ya lita 20 kwa Shilingi 1000 hali ambayo haijawai kutokea .
Tamko hilo limetolewa kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Newala baada ya Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais kazi Maalum George Mkuchika kuwasilisha hoja ya hali ya Maji ilivyofikia mpaka sasa.
Mbunge wa Newala Mjini George Mkuchika alisema, kwa miaka mingi Wakazi wa Newala wamekuwa wakipata shida ya Maji tangu enzi za mkoloni na ndipo ilipoanzishwa Mradi wa ya Makonde ili kukabiliana na tatizo la maji kwa kipindi hicho.
Amesema Serikali ya awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipobaini kuwa kuna kampuni ya watu wa Newala ambayo ilikuwa inauza maji , aliamuru Mradi wa maji wa Makonde uwe mradi wa Kitaifa na uchukuliwe na Serikali na kuwahudumia wananchi wote, japo Mradi huo umekuwa ukiporomoka poromoka kila mwaka.
“Baada ya kuona Hali ya Maji Wilaya ya Newala inaporomoka poromoka kila mwaka, na wakati mwingine wakati Nagombea Ubunge Maji huwa yanapatikana kwa asilimia 60, Wabunge wote wa Mtwara tulikubaliana kuonana na Waziri wa Maji na tukampa kilio chetu, Waziri wa Maji akamtuma Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na tukakagua Mradi wa maji Mitema na tukakuta maji yanamwagika na umeme unafanya kazi “
“Kwa sasa watumiaji wa Maji kwa Newala wameongezeka na kwenye ziara ya katibu mkuu wa Wizara aliwaleta watendaji na walihakikisha na watatengeneza na Maji yakapatikana, ila sijui nini kilitokea sijui mitambo imeharibika? Maji hayatoki na hali imekuwa mbaya, ni kweli tunashida kubwa ya maji Newala” alisema Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini George Mkuchika ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum.
Mkuchika amesema kuwa, Serikali imeiagiza Wizara Maji bila kusubiri mkopo wa Fedha, Wachukue hatua wanazoweza ili kunusuru hali mbaya ya Maji iliyopo katika Wilaya ya Newala kwenye mradi wa Makonde. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaji Mwangi Kundya alisema kuwa, Hali ya Maji ya Wilaya ya Newala ni Mbaya sana na haielezeki na Mashine za kusukuma maji zilifungwa na kuanza kufanya kazi 1954 hali zake ni mbaya na zimekuwa chakavu na mabomba yanayosafirisha maji pia yanapoteza maji njiani kabla hayajafika kwa Mtumiaji na yanayofika ni Nusu ya yale yanayozalishwa.
Ameongeza kuwa Newala hakuna Shida ya vyanzo vya Maji maji yapo yakutosha, maana chanzo cha Maji Mitema, utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa chanzo kile kinaweza kuhudumia watu Milioni 3, na kama hao watu Milioni 3 watatumia maji hayo mfululizo mpaka kufikia Mwaka 2040 watakuwa wametumia maji asilimia 15 tu ya maji. Mkoa mzima wa Mtwara una idadi ya watu Milioni 1.6 tu, kwahiyo inaweza ikanywesha Mtwara yote bila kukosekana maji.
Tatizo ni namna gani tunayatoa maji kwenye chanzo na kuyafikisha kwa watumiaji.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Makonde Mhandisi Emanuel Konkomo amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala inakadiriwa kuwa na idadi ya watu Laki Moja, ambao kwa siku moja wanahitaji maji Mita za ujazo 4,800, lakini miundombinu ya maji endapo hakuna changamoto ya umeme au mabomba kupasuka, uwezo uliopo wa kuwapelekea maji ni Mita za Ujazo 1,600 .
Serikali ya Wilaya imeshapeleka nyaraka mbalimbali za kuhakikisha wanatatua Tatizo la Maji kwa wakati, Mhandisi Konkomo amewahaidi wananchi wa Newala kuwa Mwaka wa Fedha wa mwakani watakuwa wameshakamilisha tatizo la Maji kama Mapendekezo yao yatakuwa yameingizwa kwenye mpanzo wa utekelezaji wa Wizara,