Jamii FM
Wakulima washauriwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa ya hewa wa kilimo
2 December 2022, 17:32 pm
Na Mussa Mtepa
Wakulima wameshauriwa kuacha kilimo cha mazoea na kuanza kufuata taratibu zinazoelekezwa na wataalamu wa kilimo.
Akizungumza na Jamii fm Radio afisa utabiri wa hali ya hewa kutoka kituo cha utafiti na kilimo TARI Naliendele Omari Rashidi Kahoki amesema kuwa kwa miaka ya hivi karibu kumekuwa na mvua za chini ya wastani na wastani ambazo kiuhalisia ni mvua ndogo ambazo wakulima wanatakiwa kuzitumia ipasavyo na kufuata kile wataalamu wa hali ya hewa na kilimo wanacho waelekeza.