Mzazi mhimili wa mienendo kwa mtoto wa kike
1 March 2023, 16:30 pm
Na Musa Mtepa
Wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto wa kike kwa kufuatilia minendo na tabia zao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kama wazazi kwa Watoto wao.
“Wazazi wanatakiwa kutoa chakula kwa ajili ya vijana ili waweze kupata Elimu iliyo bora kwa kufunya hivyo utakuwa umehakikisha kijana anakwenda kupata Elimu iliyo bora huku akisistiza kwa shule zote za msingi na sekondari zilizopo katika kata ya Naliendele.”
Akizungumza kwenye wiki ya Elimu iliyofanyika Shule ya Sekondari Naliendele Diwani wa kata ya Naliendele Masudi Dali amesema kuwa ili kufikia malengo ambayo yamekusudiwa kama wazazi kwa watoto.
Wazazi wanatakiwa kutoa chakula kwa ajili ya vijana ili waweze kupata Elimu iliyo bora kwa kufunya hivyo utakuwa umehakikisha kijana anakwenda kupata Elimu iliyo bora huku akisistiza kwa shule zote za msingi na sekondari zilizopo katika kata ya Naliendele.
Akizungumzia changamoto ya uwepo wa baadhi ya watoto kuandika Barua ya kuacha masomo Afisa Elimu kata ya Naliendele Benjamini Ndosi amesema kuna baadhi ya Wanafunzi wamejitokeza wa kidato cha Kwanza kwa mwaka 2023 na vidato vya juu mzazi kufika ofisini wakiambatana na Mwanafunzi wakiwa na Barua ya kuacha shule ili akajiunge na ufundi.