Mpanda FM

Wananchi Makongolo Walia na Ukosefu wa Maji

4 April 2023, 5:55 am

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Makongolo kata ya magamba halamshauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kwa kushindwa kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa kikwazo katika shughuli zao za kila siku.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa ukosefu wa maji imekuwa kikwazo hasa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Zeno Saidy amekiri uwepo wa changamoto hiyo huku akisema kikwazo kinatokana na baadhi ya wananchi kugomea kuchangia pesa kwa ajili kukamilisha upatikanaji wa maji .

Kijiji cha Makongolo ni miongoni wa vijiji vilivyopo katika kata ya Magamba Manispaa ya Mpanda huku wananchi wa eneo hilo wakikiri kukumbana na changamoto mseto za kimaendeleo.