Mpanda FM

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Alia na Matukio ya Ulawiti, Usagaji, Ushoga na Ukatili.

4 March 2023, 6:12 pm

KATAVI

Mkuu wa mkoa Wa Katavi Mwanamvua Hoza mrindoko amelitaka Jeshi la Polisi Mkoani Katavi kupitia Kitengo cha dawati kuandaa mikakati ya Kupambana na Matukio ya unyanyasi wa kijinsia kwa watoto na ulawiti yanayoendelea kushika kasi mkoani Katavi.

Akizungumza Katika Ufunguzi wa Kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa wa Katavi Mrindoko amesema umefika wakati wa kuanza kuyasemea bila kuficha ili kuyakomesha na kuzitaka mamlaka zinazohusika kukomesha vitendo hivyo.

Aidha Mrindoko Amesema tayari serikali ya Mkoa imeanza kuchukua hatua za kuthibiti matendo hayo ikiwemo kuyafungia mabweni bubu, vituo vya kulelea watoto (day care) na kuitaka Jamii mkoani Hapa kutoa taarifa waonapo vishiria vya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Kwa upande wa jeshi la Polisi Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ACP ali Hamadi Makame amesema Kupitia dawati la jinsia wamekua wakitoa elimu huku akiitaka jamii kutolea taarifa mapema mara baada ya kuona viashiria vya unyanyasaji Kwa watoto.

Hivi Karibuni Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph aliagiza kufungwa kwa kituo cha New Light Day Care na mkurugenzi wa kituo hicho kushikiliwa kwa upelelezi kufuatia kitendo cha ukatili wa kingono kilichofanywa na mwalimu wa kituo hicho sambamba na kukosa usajili.