Madiwani wahoji kutokamilika miradi, miundombinu jengo la halmashauri Tanganyika
1 February 2024, 4:48 pm
Wamehoji kutorekebishwa Kwa baadhi ya Vyoo katika Jengo Hilo Kwa muda mrefu ambavyo vimeharibika, kucheleweshwa Kwa fedha za umalizaji Shule na Zahanati ambazo zimetumia nguvu za wananchi. Picha na Festo Kinyogoto.
Na Festo Kinyogoto-Katavi
Baraza la Madiwani halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani katavi wamehoji kutorekebishwa Kwa baadhi ya miundombinu katika jengo la halmashauri pamoja na changamoto za afya na elimu
Hoja hizo zimeibuka kufuatia taarifa ya fadha elimu na Afya zilizowasilishwa ambapo Madiwani wamehoji kutorekebishwa Kwa baadhi ya vyoo katika Jengo Hilo Kwa muda mrefu ambavyo vimeharibika, kucheleweshwa Kwa fedha za umalizaji Shule na Zahanati ambazo zimetumia nguvu za wananchi, kutokuwepo Kwa Meza katika ukumbi wa Halmashauri changamoto iliyopo Kwa muda mrefu ,pamoja na Madiwani kutumia majoho yaliyochoka.
Sauti ya Madiwani wakihoji kuhusu miundombinu katika jengo la Halmashauri pamoja na changamoto za Afya na Elimu katika Halmashauri hiyo.
Akijibia hoja hizo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Juma Shabani amesema tayari halmashauri imetenga zaidi ya shilingi milioni 300 kwaajili ya ukarabati wa Miundombinu ya ukumbi wa Mikutano na kuhusu majoho ya Madiwani ameahidi utekelezaji wake utakamilika Baraza litakalofuata.
Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Juma Shabaniakijibia kuhusu changamoto zilizoibuliwa na Madiwani wakati wa Baraza hilo.
Baadhi ya watumishi wa Idara tofauti wilaya ya Tanganyika wakiwa wanasikiliza na kujibu hoja ambazo zinahusu maeneo ambayo wanasimamia.Picha na Festo Kinyogoto.
Theodora Kisesa Diwani viti maalumu Kata ya Mwese akihoji kuhusu changamoto ya bima za Afya zinazigharamiwa na Mradi wa hewa ukaa wilayani humo kutofanya kazi katika mfumo.Picha na Festo Kinyogoto.
Kuhusu watumishi Wa afya ambao wanaajiliwa katika kata mbalimbali na kuwekwa hospitali ya Wilaya Kwa muda bila kwenda maeneo husika Madiwani wameshauri kupelekwa vifaa Maeneo husika ili waajiliwa waende katika maeneo Yao ya kazi pamoja na magari ya wagonjwa kupelekwa katika maeneo ya mbali kama Kalema na mwese.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema wanafanya hivyo kwakuwa wagonjwa wengi na rufaa zipo katika hospitali ya Wilaya, hivyo wanafikishwa hapo kwaajili ya kuwaandalia mazingira Bora ya kazi katika maeneo wanayo ajiliwa na pindi mazingira yanapokamilika wanapelwkwa maeneo husika.
Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Juma Shabania kijibia kuhusu Watumishi walioajiliwa katika kata mbalimbali kubakishwa hospitali ya wilaya.
Mkurugenzi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Juma Shabani wakati akitoa majibu ya hoja ambazo ziliulizwa na madiwani wakati wa baraza hilo.Picha na Festo Kinyogoto