Katavi yaongoza kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania
20 December 2023, 4:43 pm
Viongozi,watendaji na wadau mkoani Katavi wameaswa kuyatumia vizuri Matokeo ya sensa ya sita ya watu na makazi iliofanyika mwaka 2022 katika kutimiza adhma ya serikali
Na Festo Kinyogoto – Katavi
Mkoa wa Katavi unaongoza Kwa kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania
Viongozi,watendaji na wadau mkoani Katavi wameaswa kuyatumia vizuri Matokeo ya sensa ya sita ya watu na makazi iliofanyika mwaka 2022 katika kutimiza adhma ya serikali ya kutekeleza shughuli za kimaendeleo.
Hayo yamesemwa na mgeni rasmi Onesmo Buswelu akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kikao Cha mafunzo ya usambazaji na matumizi ya Matokeo ya sensa ya watu na makazi Kwa viongozi, watendaji na wadau mkoani Katavi ambapo amesema Matokeo hayo ndio Muongozo sahihi wa shughuli zote zinazotakiwa kutekelezwa.
Muwakilishi kutoka katika ofisi ya takwimu ya taifa NBS Lusy Minja amesema mkoa wa Katavi umeongoza Kwa kuwa na ongezeko la watu mara mbili zaidi nchini Tanzania, hivyo mipango lazima iakisi ongezeko la watu ili kukidhi idadi na ustawi wa Maisha ya wananchi.
Aidha Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa mkoa wa pili Kwa idadi kubwa ya watoto ikiwa na asilimia 56 nyumaa ya Simiyu yenye asilimia 57.
Kikao hicho kimelenga kutumia takwimu za ongezeko Hilo katika kuendana na kasi ya ongezeko la watu Kwa mujibu wa takwimu katika huduma zote za kijamii, uchumi,afya umeme, maji, elimu siasa na utamaduni huku kuzaliana uhamiaji na Hali ya kiuchumi zikitajwa kama sababu za ongezeko Hilo.