Mrindoko: Serikali itaendelea kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo vya uharifu
11 October 2023, 3:55 pm
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema serikali mkoani hapa itaendelea kuwachukulia hatua kali wahusika wote wa vitendo vya uharifu.
Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Marindoko amesema kuwa serikali mkoani hapa itaendelea kuwachukulia hatua kali wahusika wote wa vitendo vya uharifu ikiwemo wizi wa kutumia nguvu ili kuendelea kulinda usalama wa raia na malizao.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na vyombo vya Habari kufuatia vitendo vya kiharifu ambavyo vinaendelea kujitokeza katika maeneo ya mbalimbali ya mkoa wa Katavi likiwemo tukio la wizi wakutumia nguvu ambalo limejitokeza usiku wa kuamkia October 4 katika manispaa ya Mpanda.
Kwaupande wake Kamanda wa polisi Mkoani hapa Castar Ngoyani amezungumzia juu ya matukio mbalimbali yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali katika Mkoani hapa amesema kuwa matukio mengi yanayo jitokeza yanatokana na wivu wa mapenzi sambamaba na usaliti katika biashara.
Aidha Mrindoko akizungumza juu ya tukio la mauwaji ya Watoto wawili katika jitongoji cha kabatini kata ya mwese amesema kuwa jumla ya watu watano wananendelea kushikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa uchunguzi zaidi.