Mpanda FM

Kizungumkuti Barabara ya Kabungu – Karema

29 August 2023, 10:05 am

TANGANYIKA.

Baadhi ya Wananchi Mkoani Katavi wanaotumia Barabara ya Kabungu kwenda Karema wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara hiyo na kuitaka serikali kuifanyia matengenezo kwa kiwango cha lami.

Wakizungumza na mpanda redio fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wameleeza kuwa barabara hiyo imekuwa korofi kwa watumiaji ,ambapo wameitaka serikali kutimiza ahadi yake ya kuijenga kwa kiwango cha lami kama ambavyo viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa ahadi kuhusu barabara hiyo.

Meneja wa wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Katavi injinia Martin Mwakabende amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwani barabara hiyo ipo katika hatua ya mwisho kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami ambapo tayari hatua iliyopo kwa sasa ni hatua ya manunuzi.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 112 ni moja ya barabara muhimu katika mkoa wa Katavi kwani ndiyo kiunganishi cha Bandari ya karema inayopatikana katika wilaya ya Tanganyika mkoani hapa .

#mpandaradiofm97.0

#tanroads