Jamii FM

Makala: Mwitikio wa wanawake kugombea nafasi za Uongozi

26 December 2024, 15:53 pm

Brandina Chilumba ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mihambwe kwenye kata ya naliendele. Picha na Mwanahamisi Chikambu

Na Mwanahamisi Chikambu pamoja na Gregory Millanzi

Tanzania imeandika historia kwa kuwa moja ya nchi chache zilizoongozwa na Rais mwanamke, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Miaka 63 tangu kupata uhuru kutoka kwa Mkoloni Mwingereza, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekua Rais wa kwanza mwanamke wa taifa hili, hatua iliyochochea ari mpya miongoni mwa wanawake wengi kushiriki kikamilifu katika siasa na kugombea nafasi za uongozi.

Uongozi wa Rais Samia umeibua matumaini mapya na kuwahamasisha wanawake kujiamini zaidi katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi, hususan zile za kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi. Katika mkoa wa Mtwara, mwitikio wa wanawake katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024, umeonyesha dalili nzuri za mabadiliko. Wanawake wengi wamejitokeza kugombea nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa, wakionyesha utayari wa kushiriki katika maendeleo ya jamii na kutetea maslahi ya wananchi kwa ujasiri.

Makala hii inatoa taswira ya namna mabadiliko haya yanavyoashiria ongezeko la ushiriki wa wanawake katika uongozi na hatua zinazochukuliwa kuendeleza usawa wa kijinsia katika ngazi zote za utawala.

Bonyeza hapa kusikiliza