Jamii FM

Upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wenye ulemavu

24 December 2024, 15:34 pm

Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la MSOAPO Ndugu Mustafa Kuyunga akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano. Picha na Msafiri Kipila

Na Msafiri Kipila na Grace Hamis

Abedi Yusuph Lukanga ambaye ni mlemavu wa miguu, amesema kwamba bado kuna changamoto kubwa katika huduma za afya na za kijamii kwa watu wenye ulemavu kutokana na miundombinu isiyo rafiki kwa mahitaji yao. Hata hivyo amepongeza baadhi ya watoa huduma za afya kwa kumwelewa na kumhudumia vizuri katika sehemu kadhaa.

Kwa upande wake, Siwema Yusuph Lukanga mtoto wa Abedi, amesema anakutana na changamoto kubwa wakati wa kutafuta huduma za afya kwa mpendwa wake. Ameomba Serikali kuweka mpango wa bima ya afya kwa watu wenye ulemavu ili kupunguza changamoto hizi.

Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la MSOAPO, Mheshimiwa Mustafa Kuyunga amesema kuna mapungufu makubwa katika upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu, hasa miundombinu isiyo rafiki na ucheleweshaji wa huduma.

Aidha, amesema shirika lao linaendelea kutoa elimu na kushawishi Serikali kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu. Amewapongeza juhudi za Serikali katika kuinua hali ya watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapata huduma bora za afya, lakini amesisitiza haja ya kuimarisha zaidi juhudi hizo.

Bonyeza hapa kusilikiza