Makungwi Mtwara Kuwacheza Watoto unyago Kuanzia Miaka Kumi
2 November 2024, 21:13 pm
Na Mwanahamisi Chikambu
Makungwi mkoani Mtwara wamependekeza kuwacheza watoto kuanzia umri wa miaka kumi na kuendelea ili watoto waweze kuelewa wanayofundishwa katika jando na unyago na kuacha kufundisha mila potovu ambazo hazileti tija kwa jamii.
Wameyasema hayo katika kikao cha mpango mkakati kupitia mradi wa kuwezesha wasichana na kupaza sauti na kujadili changamoto zao leo November mosi 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa TCCIA mkoani Mtwara.
Sophia Ally Chilindu kutoka wilaya ya tandahimba ,Fatuma issa kutoka shangani ,Ziada Daniel kutoka wilaya ya masasi na Halima kaidi kutoka Newala vijijini katika kijiji cha lengo wameelezea namna ya walivyokuwa wanawafundisha watoto kabla ya kupata mafunzo kutoka kwa Shirika la Sports Development Aid (SDA) na namna ambavyo wanavyofundisha kwa sasa baada ya kupata mafunzo hayo.
Makungwe hao wamesema kupitia mradi huo wamenufaika na mambo mengi ikiwemo kuongeza uwezo wa watoto wa kike kuweza kujiamini na kufanya vizuri kwenye masomo yao, kupunguza utoro mashuleni kutokana na uwepo wa michezo na vifaa vya michezo vilivyotolewa na shirika hilo , kupunguza vitendo vya ukatili kutokana na elimu iliyotolewa kupitia matamasha yaliyofanywa na shirika hilo, na kuboresha mafunzo wanayopewa watoto wanaochezwa ngoma huku wakiahidi kuyaendeleza.
Aidha kwa upande wake afisa utamaduni wa manispaa mtwara mikindani Arsula Kayombo amewashukuru Shirika la Sports Development Aid (SDA) kwa kuwapatia makungwi mmafunzo ambayo yanafana katika mkoa mzima wa mtwara ambayo yataleta tija kwa jamii.
Kwa upande wake afisa maendeleo wa manispaa mtwara mikindani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika katika kikao cha mpango mkakati kupitia mradi wa kuwezesha wasichana na kupaza sauti na kujadili changamoto zao amewataka makungwi hao kuendeleza yale ambyo wamejifunza katika mafunzo mbalimali ambo yaliuwa yakitekelezwa na Shirika la Sports Development Aid (SDA.
Mkurugenzi wa Shirika la Sports Development Aid (SDA) Thea Swai amesema kuwa kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani uwelewa wa makungwi ulikuwa ni mdogo kwa sababu elimu ambayo walikuwa wanazitoa hapo awali i kwa watoto imepita na wakati.