Jamii FM

Shamsia aongoza kampeni za CUF Mnaida, Mtwara

25 November 2024, 07:48 am

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini akiwanadi wagombea wa nafasi za uenyekiti ,wajumbe kwa wananchi wa kijiji cha Mnaida (Picha na Musa Mtepa)

Hizi ni kampeni za vyama vya siasa ikiwa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024 kote nchini ambapo hivi sasa vyama vina nadi sera zao kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa.

Na Musa Mtepa

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Mh. Shamsia Mtamba, Novemba 24, 2024, amewataka wananchi wa Kijiji cha Mnaida na Kata ya Tangazo kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwachagua viongozi wanaotokana na chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza kama mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kupitia CUF, Mh. Mtamba amesema kuwa yeye anahubiri kampeni za kistaarabu ambazo zimejaa matumaini kwa wananchi huku akielezea dhamira yake ya kutatua kero zinazowakabili wananchi na kuendelea kuweka alama katika kila kata ya Jimbo la Mtwara Vijijini.

Sauti ya 1 Shamsia Aziz Mtamba Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini

Aidha, Mh. Mtamba amewataka wananchi wa Kijiji cha Mnaida kuendelea na mapambano ya kuhakikisha wanapata wenyeviti wa vijiji na vitongoji kutoka chama cha CUF ili kumrahisishia njia ya kuendelea kuwa mwakilishi katika uchaguzi mkuu ujao.

Sauti ya 2 Shamsia Aziz Mtamba Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Mtwara, Abdul Mahupa, amesema kuwa changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa 2019, ambapo viongozi wengi wa vijiji walichaguliwa kutoka chama cha CCM, zimepelekea kukwama kwa miradi mbalimbali.

Mahupa amesisitiza kuwa ili miradi hiyo iweze kukamilika, wananchi hawana budi kuchagua viongozi kutoka CUF.

Sauti ya 1 Abdul Mahupa mwenyekiti wa CUF wilaya

Aidha, Mahupa ameeleza kuwa vijijini kumekuwapo na madudu mengi ambayo yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya wananchi, kutokana na kuegemea zaidi siasa za chama badala ya kuzingatia maendeleo ya wananchi.

Sauti ya 2 Abdul Mahupa mwenyekiti wa CUF wilaya

Katika mkutano huo, Juma Mega, mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Kijiji cha Mnaida, pamoja na baadhi ya wagombea wa nafasi za uenyekiti wa vitongoji, wameomba kura mbele ya wananchi waliojitokeza.

Sauti ya wagombea ya nafasi ya uenyekiti wa Kijiji na vitongoji