Miaka 62 hakuna mtoto aliyesoma darasa la awali
5 November 2024, 16:47 pm
Na Gregory Millanzi/ Mwanahamisi Chikambu
Miaka 62 iliyopita tangu kupata uhuru wa nchi ya Tanganyika na baadae kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kijiji cha Ngorongoro kata ya Nanguruwe Halamashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani hapa, hakijawahi kuwa na wanafunzi waliosoma elimu ya awali kutoka kijijini hapo kutokana na umbali wa Shule ya awali na msingi ambayo ipo Kilomita 5 toka kijijini hapo hadi makao makuu ya kata ya Nanguruwe.
Baada ya hali hiyo kuwa kikwazo kwa watoto wao kupata elimu ya darasa kwa miaka mingi, kupitia uongozi wa Mwenyekiti wa kijiji hicho Said Athumani Ngulyungu kwakushirikiana na wanakijiji waliamua kuanza mchakato wa kuanzisha shule shikizi hasa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wa kilomita 5 kufuata shule.
Kusikiliza Makala haya Bonyeza Hapa
Je Ungependa kufahamu Kuhusu Jamii FM? bonyeza hapa