Nuru FM

Wanabari pingeni ukeketaji

15 March 2021, 10:59 am

Waandishi wa habari wa redio za jamii nchini wametakiwa  kuelimisha jamii juu ya kupinga ukeketaji na ndoa za utotoni  dhidi ya wanawake na watoto

hayo yamezungumzwa na afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Arusha Angela Kiama Mvaa katika mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu ukeketaji kwa wanawake na watoto  yaliyoandaliwa  na  shirika la C-Sema  kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa UNFPA ambapo amewataka wanahabari kuwa sauti ya kukemea masuala hayo husasani maeneo ya vijijini.

CDO ARUSHA ANGELA KIAMA
SAUTI 1 CDO ANGELA KIAMA

WARREN BRIGHT  ni afisa uhusiano  wa UNFPA amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wandishi wa redio jamii nchini wanapata mbinu bora za kuandaa vipindi dhidi ya ukeketaji kwa wanawake na watoto

KWA upande wake   Michael Marrwa kutoka shirika la C-Sema  amewataka wanahabari kuelimisha jamii juu ya ukatili kwa watoto kwa kuwa watoto huweka visasi na kuathirika kisaikolojia pia.