MPANDA,Homa ya Ini Yaongezeka kwa Kasi
7 March 2024, 3:09 pm
“Daktari wa Manispaa ya Mpanda Coronel Bruno amesema kuwa ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia kupima Afya kila mara ili kubaini.” Picha na Mtandao.
Na Veronica Mabwile-katavi
Baadhi ya Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba Serikali mkoani Katavi kuongeza jitihada za utoaji wa Elimu juu ya Magonjwa ya Kuambukiza ikiwemo Ugonjwa wa Homa ya ini ili kuongeza uelewa kwa Wananchi.
Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia uwepo wa ongezeko la ugonjwa huo na kusema kuwa namna ya kutokomeza Ugonjwa huo ni pamoja na Wananchi kupewa elimu ya kutosha juu ya dalili za Ugonjwa huo na namna ya kujikinga.
“Sauti za wananchi wakizungumza kuhusu uelewa wao Juu ya homa ya Ini na hatua gani zichukuliwe ili kukabiliana nao”
Akizungumza Wakati wa kongamano la Wanawake daktari wa Manispaa ya Mpanda Coronel Bruno amesema kuwa ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia kupima Afya kila mara ili kubaini
“Sauti ya Daktari wa Manispaa ya Mpanda Coronel Bruno alipokuwa akizungumza katika kongamano la Wanawake kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani kuhusu sababu za kuongezeka kwa ugonjwa huo”
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na Mcho kubadilika rangi na kuwa ya Njano, kupungua Uzito, hamu ya kula ,pamoja na ngozi ya Mwili kuwasha.