Mpanda FM
Mifumo Mibovu ya Maisha Chanzo cha Magonjwa Yasiyoambukiza
20 November 2021, 10:44 am
Wananchi mkoani katavi wameshauliwa kubadili mtindo wa maisha ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo.
Kauli hiyo imetolewa na daktari wa idara ya magonjwa yasiyoambukiza kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi dokta Daniford Mbohilu akifanya mahojiano na mpanda redio fm na kusema matatizo ya moyo husababishwa na mtindo wa maisha ambao watu wanaishi bila kuzingatia utaratibu wa kiafya.
Aidha Mbohilu amewataka watu kuishi maisha yenye afya na kuwa na tabia ya kuchunguza afya mara kwa mara, pia kuzingatia ufanyaji wa mazoezi ili kupunguza uzito uliozidi mwilini.
Kila ifikapo tarehe ishirini na tisa ya mwezi wa tisa kila mwaka dunia huazimisha siku ya moyo. яндекс