Nuru FM

Ukaguzi Vyombo vya Moto kwa Hiyari

16 February 2023, 5:07 pm

Mratibu wa polisi mkoa wa Iringa Mosi Ndozero kulia pamoja na Mkaguzi wa magari na Mtahini Afande Issack katikati wakiwa katika studio za Nuru Fm wakieleza kuhusu ukaguzi vyombo vya moto kwa hiari. Picha na Elizabeth Shirima

Kufuatia wiki ya nenda kwa usalama ambayo imeanza kuadhimishwa kitaifa kuanzia Februari 6, 2023 ambapo Mkoani Iringa itazinduliwa mnamo Februari 18, 2023.

Na Ansigary Kimendo.

Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani Mkoani Iringa limejipanga kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto kwa hiyari, katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo yanatarajiwa kuadhimishwa kuanzia tarehe 18 februari 2023.

Akitaja maeneo ambayo zoezi hilo litafanyika Mratibu wa polisi Mkoa wa Iringa Mosi Ndozero amesema kuwa ukaguzi utaenda sambamba na utoaji stika za wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Mratibu wa polisi Mkoa wa Iringa Mosi Ndozero akieleza maeneo ambayo tukio la ukaguzi wa hiyari utafanyika

Aidha amewataka waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kuwa watii wa sheria bila shuruti ili kupunguza ajali ambazo zinatokana na uvunjifu wa sheria.

Mratibu wa polisi Mkoa wa Iringa Mosi Ndozero akitoa wito kwa madereva wa pikipiki (bodaboda)

Kwa upande wake Mkaguzi wa magari na Mtahini Afande Issack amesema kuwa katika kuendeleza ukaribu na wananchi wamekuwa wakifata vyombo vya moto kwaajili ya kufanya ukaguzi.

Mkaguzi wa magari na Mtahini Afande Issack akieleza namna kitengo cha Usalama Barabarani kinavyofanya kazi