Nuru FM

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi aapishwa kuanza majukumu yake

4 February 2023, 10:35 am

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Linda Selekwa akila Kiapo cha uadilifu

Nendeni Mkawe mstari wa mbele kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi wenu ili kumrahisishia kazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na Joyce Buganda

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Linda Selekwa  kuanza majukumu yake baada kuteuliwa hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa Kiapo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego Amesema kuwa ni vyema viongozi walioteuliwa wakawa mstari wa mbele kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego akizungumza wakati wa kumuapisa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi

Aidha Mh. Dendego amewataka Wakuu wa Wilaya kuacha alama katika utekelezaji wa majukumu yao ili wananchi wajivunie kuwa na viongozi wenye uadilifu.

“Ninakusihi kuhakikisha unasimamia maadili katika kuwatumikia wananchi wa Mufindi ili kukuza uchumi wa Wilaya hiyo, nenda kashirikiane na viongozi wenzako ili mfikie lengo” Alisema Dendego

“Ninakusihi kuhakikisha unasimamia maadili katika kuwatumikia wananchi wa Mufindi ili kukuza uchumi wa Wilaya hiyo, nenda kashirikiane na viongozi wenzako ili mfikie lengo” Alisema Dendego

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mufindi LINDA SELEKWA amewaomba  viongozi pamoja na wananchi kumpa ushirikiano  muda wote atakaokuwa katika majukumu yake ya kiutendaji.