Nuru FM

Wananchi iringa wahimizwa kufunga mwaka kwa kufanya utalii wa Kulisha wanyama

12 December 2022, 11:14 am

Kampuni ya usafirishaji watalii ya Bateleur Safari & Tours Mkoa wa Iringa inatarajia kufanya ziara ya utalii ya kufunga mwaka 2022.

Akizungumza na Nuru Fm, Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Rajipa David amesema kuwa kuelekea kufunga mwaka 2022 wameandaa Ziara iliyopewa jina la Tukalishe Twiga ambayo itafahusisha watalii kutoka Iringa na Dodoma kuanzia tarehe 31/12/2022.

“Siku ya kwanza tutakuwa na watalii kutoka Iringa na Dodoma Kwa ajili ya kwenda Arusha na Kisha kuelekea Moshi eneo la sanya Juu Kwa ajili tukio la kulisha wanyama” alisema Rajipa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya usafirishaji watalii ya Bateleur Safari & Tours Mkoa wa Iringa Rajipa David akiwa katika Utalii wa Kulisha wanyama aina ya Twiga.

Amesema kuwa Mtalii anaweza kupiga Picha na wanyama Hao Kwa kuwa wamepewa mafunzo maalumu hivyo  amewatoa hofu wale wanaohitaji kujiunga katika ziara Hiyo.

Aidha amesema kuwa siku Hiyo wataenda kufanya ziara Katika kivutio Cha Chemka Kwa ajili ya maji moto na katika Mlima Kilimanjaro.

Rajipa amesema kuwa zoezi Hilo litafanyika siku ya Pili ya tarehe 1/1/2023 ambapo Kwa wale ambao wanataka kushiriki katika ziara Hiyo ya utalii wa kulisha wanyama ni shillingi Laki Tano na elfu hamisini. (550,000/=) Kwa mtu mmoja.

 

“Gharama Hiyo itahusisha usafiri Kwa wanaoanzia Iringa na Dodoma, chakula, malazi katika hotel zote Ndani la Jiji la Arusha, gharama za kiingilio kwenda kwenye site zote, nyama choma na gharama za picha” alisema Rajipa.

Amesema Kwa wale wanaohitaji kushiriki katika ziara Hiyo ya utalii wanaweza kumpigia Kupitia namba za simu za 0765735261 Ili kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka Kwa kishindo.

 

PICHA ZA MATUKIO  MBALIMBALI YANAYOHUSU UTALII WA KULISHA WANYAMA