Nuru FM

Watahiniwa 566,840 kuanza mtihani kidato cha nne kesho

13 November 2022, 11:20 am

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limesema jumla ya watahiniwa 566, 840 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, utakaoanza kesho Jumatatu katika shule za Tanzania Bara na Zanzibar.

Limesema kati yao watahiniwa 533,001 ni shule na 31, 839 wa kujitegemea .Kati ya hao watahiniwa wavulana ni 247,131 sawa na asilimia 46.19 na wasichana 287,870 sawa na asilimia 53.81.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi, ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mtihani huo, akisema kila kitu kinakwenda vizuri ikiwemo mitihani kufika kwenye mikoa na vituo husika.

Amasi amesema katika idadi hiyo wapo watahiniwa wenye mahitaji maalumu 852 kati ya 480 wana uhoni hafifu, 62 wasioona, 19 wenye ulemavu wa kusikia, 152 wenye mtindio wa akili na 139 wana ulemavu wa viungo.

“Mwaka 2021 idadi ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 538,024 hivyo kuja ongezeko la jumla ya watahiniwa 28,816 sawa na asilimia 5.36 kwa mwaka 2022 ukilinganisha na mwaka 2021.

“Maandalizi ya mtihani huu wa kesho yamekamilika ikiwa ni pamoja kusambazwa kwa mtihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani katika mikoa ya Tanzania na Zanzibar,” amesema Amasi.

Amasi amesema mtihani wa kidato cha nne ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa sababu ina pima umahiri wa wanafunzi katika masomo yote aliyojifunza kwa muda wa miaka minne.Pia amesema matokeo ya mtihani huo yanatumika katika chaguzi za wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu ya sekondari na fani mbalimbali