Nuru FM

Rc Manyara Awapa Kazi Takukuru Kuchunguza Kilombero

17 September 2022, 7:16 am

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mashamba yaliyouzwa na kugawanywa kwa wananchi na kuchangishwa sh60,000 kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.

Makongoro akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kilombero amesema Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Severin Nombo na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Simanjiro Oliech Otenyo.

 

“Sijatoa muda maalum ila TAKUKURU chunguzeni hayo mashamba yalivyogawanywa na mchango wa sh60,000 wa kujenga zahanati ulivyotumika,” amesema Makongoro.

Amesema wananchi wa kijiji hicho wanalalamikia kuwa wamechangishwa sh60,000 na pia kuna baadhi ya mashamba yamegawanywa na kuuzwa na fedha hizo kuingizwa kwenye ujenzi huo

 

Pia amesema Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt Suleiman Hassan Serera atafuatilia uhalali wa ekari 2,000 zilizotolewa kwa mtu mmoja katika kijiji cha hicho.

 

Diwani wa kata ya Shambarai Julius Mamamsita amepongeza hatua hiyo kwani wananchi wamelalamikia hilo kwa muda mrefu.

 

Mkazi wa kijiji hicho Michael Kilusu amemshukuru Mkuu huyo wa mkoa kwa kuagiza uchunguzi huo ili ukweli ubainike.