Bustani Jiko Mkombozi wa Udumavu
19 November 2021, 11:52 am
Wananchi Mkoani Katavi wameaswa kujihusisha na kilimo cha Bustani Mkoba ili kuepukana na changamoto ya utapiamlo na udumavu unaosababishwa na ulaji usiofaa
Hayo yameelezwa na Gastor Mwakilembe Afisa Kilimo Manispaa ya Mpanda ambae pia ni Mratibu wa mradi wa Bustani Jikoni mkoani hapa wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm ambapo amesema kuwa baadhi ya familia zimekuwa zikitumia mlo wa aina moja.
Aidha Afisa lishe kutoka MICO Fikirio Gambi ameshauri wakulima wa mbogamboga kutumia njia za asili za kuzuia wadudu katika mbogamboga badala ya kemikali ambazo hugeuka kuwa sumu kwa mlaji zisipofatiliwa vizuri
RIKOLTO kwa kushirikiana na MICO wameanzisha mradi wa bustani jikoni ili kupunguza na ikibidi kutokomeza kabisa changamoto ya Utapiamlo na Udumavu Mkoani Katavi.