Mpanda FM
12,000 Wapata Chanjo ya Sinopharm
19 November 2021, 10:14 am
KATAVI
Zaidi ya wananchi elfu nne mkaoni katavi wamepata chanjo ya dozi ya kwanza ya sinopharm na kufanya idadi ya watu waliopata chanjo ya uviko19 kufikia elfu kumi na mbili mkoani hapa.
Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa mkoa wa katavi dr omari sukari wakati akizungumza na kituo hiki ambapo ameeleza huduma mkoba imerahisisha kuwafikia wananchi wengi kupata chanjo.
Aidha baadhi ya viongizi wa dini ,taasisi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali wamethibitisha kutokupata madhara yoyote baada yakupata chanjo ya uviko19.
Tarehe 4 mwezi wa nane mkoa wa katavi ulizindua huduma ya mpango shirikishi wenye lengo la kuwafikia wananchi wengi kupata chanjo ya uviko -19 kwa urahisi .