

10 April 2025, 3:16 pm
“Maeneo mengi ya vyanzo vya maji katika bonde hilo bado yanakabiliwa na kitisho cha uharibu wa mazingira “
Na Restuta Nyondo -Katavi
Matumizi ya mawasiliano jumuishi kwa jamii imetajwa kuwa mbinu muhimu zaidi ya kutumia usimamizi wa sheria pekee katika kukabiliana na changamoto za uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Haya yanajiri katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la uhifadhi mazingira dunaini IUCN kwa ushirikiano wa GIZ na bonde la maji la ziwa Rukwa katika utekelezaji wa mradi IKI-KATUMA unaolenga kidakio cha Mto Katuma mkoani Katavi.
Doyi Mazenzele ni meneja mradi kutoka katika shirika la uhifadhi mazingira Duniani IUCN amesema kuwa jamii ya wakulima, wafugaji na watumia maji kwa ujumla wanapaswa kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali za maji.
Afisa uhusiano kutoka bonde la maji la ziwa Rukwa Thadeus Ndese amesema kuwa maeneo mengi ya vyanzo vya maji katika bonde hilo bado yanakabiliwa na kitisho cha uharibu wa mazingira kutokana na shughuli za kibinadamu.
Nasra Nasoro ni Mtaalamu wa maji juu ya ardhi kutoka bonde la maji la ziwa Rukwa amesema mafunzo waliyopata yatasaidia katika kuyafikia makundi mbalimbali kwa urahisi zaidi ili waweze kushiriki moja kwa moja kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika halmashauri ya manspaa ya Mpanda kwa siku mbili yaliwahusisaha watalaamu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Katavi, halmashari, ,vyombo vya habari na wadau kutoka mashirika mbalimbali.