Mpanda FM

‘Wanaofanya ukatili mtandaoni wachukuliwe hatua’

8 April 2025, 12:20 pm

Picha ya Koplo Steven afisa wa dawati la jinsia na watoto Katavi. Picha na Samwel Mbugi

“Ukuaji wa utandawazi umesababisha baadhi ya wananchi kufanya ukatili pasipo kujua”

Na Samwel Mbugi

Baadhi ya Wananchi mkoani katavi wameiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu atakaebainika kufanya ukatili wa kijinsia kwenye mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikitumika katika uzalilishaji.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio FM kuwa mitandao ya kijami imekuwa ikitumika katika ukatili, ambapo baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakifanya matukio hayo, na kuto kuchukuliwa hatua za kisheria

Sauti ya wananchi

Koplo Steven ni afisa wa dawati la jinsia na watoto amesema kuwa ukatili ni tendo lolote linalofanyika kwenye mitandao ya kijamii likiwa na lengo la kumkashifu mtu au jamii.

Sauti ya koplo Steven

Pia Steven amesema kuwa kutokana na ukuaji wa utandawazi umesababisha baadhi ya wananchi kufanya ukatili pasipo kujua kama wanachokifanya ni ukiukwaji wa maadili, ambapo wahanga wakubwa ni watoto na wanawake.

Sauti ya koplo Steven

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa makini wanapotumia mitandao ya kijamii kwani ni kosa kisheria kutuma picha za utupu na kutoa tarifa za uongo.