

7 March 2025, 2:13 pm
Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere. Picha na Anna Mhina
“Wanawake wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu”
Na Anna Mhina
Wanawake mkoani Katavi wametakiwa kujitoka katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa na kuwataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu sambamba na kuwataka kuchangamkia fursa za mkopo wa asilimia kumi.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katibu wa jukwaa la wanawake mkoa Baby Mbalala ameeleza lengo la kauli mbiu kuwa ni kuhamasisha jamii kukuza usawa wa haki na uwezeshwaji.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake waliohudhuria sherehe hizo wameeleza furaha zao kwa kutambua haki zao na kupinga matendo maovu.
Sherehe hizo za wanawake kwa mkoa wa Katavi zimefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili ambapo kitaifa zinatarajiwa kufanyika mkoani Arusha na mgeni rasmi atakuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan.