Shule ya msingi Kasisiwe yakabiliwa na upungufu wa madawati
23 January 2025, 1:56 pm
Wananchi wa mtaa wa Kasisiwe wakiwa kwenye kikao. Picha na John Benjamini
“Wazazi watakiwa kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati”
Na John Benjamini
Shule ya msingi Kasisiwe iliyopo kata ya Ilembo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi inakabiliwa na upungufu wa madawati 750.
Akisoma taarifa ya shule hiyo Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kasisiwe Jane Sigarate katika mkutano wa wazazi mbele ya afisa elimu amesema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 3,000 na madawati 164 kupelekea upungufu wa madawati 750 kwa msimu wa mwaka huu wa 2025 na kuwaomba wazazi kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati.
Afisa elimu Manispaa ya Mpanda Gerad Kisiasi akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Mpanda ameleeza kuwa wazazi wanapaswa kuunda kamati kwa ajili ya kuendesha na kusimamia zoezi hilo la uchangiaji wa madawati katika shule hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wamesema kuwa wako tayari kuchangia idadi hiyo ya madawati ili kunusuru changamoto hiyo kwa wanafunzi na kuunga mkono jitihada za serikali za kuwajengea shule katika eneo hilo
Shule ya msingi Kasisiwe imeanzishwa mwaka 2024 imejengwa kwa fedha kutoka serikali kuu na hivi karibuni ilipokea madawati 68 kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda.