Bodaboda wanufaika na mikopo ya asilimia kumi
23 January 2025, 10:53 am
Picha ya viongozi pamoja na bodaboda wa halmashauri ya Nsimbo. Picha na Anna Mhina
“Bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani “
Na Anna Mhina
Mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo iliyopo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Halawa C. Malendeja amewataka madereva bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wanafuatilia utaratibu wa kupata leseni.
Mwenyekiti Malendeja ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi pikipiki kwa vijana wa halmashauri hiyo waliopokea mkopo wa asilimia kumi na amewataka kuhakikisha wanafanya utaratibu wa kupata leseni.
Wakipokea pikipiki hizo baadhi ya madereva bodaboda wameishukuru serikali kwa kuwapatia mkopo uliosaidia kununua pikipiki na kuahidi kuyatekeleza yale yote walioelekezwa na mwenyekiti.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Erimkwasi John ameeleza kuwa wamegawa pikipiki 13 kwa vikundi viwili huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Eng. Stephano B. Kaliwa akieleza malengo ya halmashauri ya mwaka wa fedha.