Wananchi washauriwa kujenga nyumba imara
16 January 2025, 1:02 pm
“Inapojengwa nyumba imara husaidia kuepusha majanga hasa tetemeko la ardhi linapotokea“
Na Roda Elias-Katavi
Wananchi manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshauriwa kujenga nyumba zilizo imara na kuzikagua kila wakati ili kuepukana na athari za tetemeko la ardhi.
Ushauri huo umetolewa na Catherine Sambagi ambae ni Afisa Habari wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoani Katavi ambapo amesema kuwa katika kuhakikisha usalama wa binadamu na mali zote ni vyema kuwa na desturi ya kukagua nyumba mara kwa mara.
Sambagi ameinisha kuwa zipo njia mbali mbali ambazo zinaweza kusaidia kuepukanana na athari za tetemeko la ardhi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari ili kuepukana na athari za majanga hayo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda wakizungumza wameitaka serikali kutoa elimu kuhusiana na tetemeko la ardhi ili waweze kuchukua tahadhari pindi majanga hayo yatakavojitokeza.
Tetemeko la ardhi linasababishwa na shughuli za kibinadamu hususani uchimbaji wa madini lakini pia tetemeko la ardhi lina Athari kama mmomonyoko wa ardhi pamoja na kuanguka kwa majengo.