Wananchi Katavi washauriwa kuweka malengo ya mwaka
9 January 2025, 9:31 am
“Kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka husaidia kuepuka matumizi yasiyoyalazima“
Na Lilian Vicent -Katavi
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wamesema kuwa kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka ni moja ya sababu inayochangia kufikia mafanikio kwa wakati.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamebainisha watu wengi wamekuwa wakiweka malengo mengi na kushindwa kuyakamilisha mpaka mwishoni mwa mwaka.
Sauti za wananchi wakizungumza
Ponisian Mtui ambaye ni mwanauchumi amesema kuweka malengo mwanzoni mwa mwaka usaidia kuepuka matumizi yasiyoyalazima iwapo utafanya tathimini juu ya suala husika.
Sauti ya Ponisian Mtui Mwanauchumi
Sanjari na hayo Posian amesema taasisi au mtu mmoja mmoja wanatakiwa kuweka malengo ili kubainisha mambo ya msingi na kuyafanyia utafiti kabla ya kuanza utekelezaji.