Mpanda FM

Kamati ya kudumu ya bunge haijaridhishwa na kasi ya ujenzi sekondari Katavi boys

8 January 2025, 8:43 pm

moja ya jengo la shule hiyo linaloendelea kujengwa.picha na John Benjamin

changamoto ambazo zinapelekea mradi huo kuchelewa kukamilika ikiwemo upatikanaji wa wadhabuni kwa vifaa

Na John Benjamin -Katavi

Kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi haijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Katavi Boys.

Kamati hiyo imeyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo mkoani Katavi ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Justin Lazaro Nyamonga amemwagiza mkuu wa mkoa wa Katavi kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinapatikana kwa wakati ili shule hiyo iweze kukamilika katika ubora uliokusudiwa ili iweze kunufaisha jamii.

Sauti ya mwenyekiti wa kamati hiyo Justin Lazaro Nyamonga

mwenyekiti wa kamati hiyo Justin Lazaro Nyamonga.picha na John Benjamin

Akisoma taarifa ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Katavi Boys mwalimu wa shule ya Kasokola inayojengwa katika kata ya Kasokola manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ameainisha changamoto ambazo zinapelekea mradi huo kuchelewa kukamilika ikiwemo upatikanaji wa wadhabuni kwa vifaa ambapo ameleeza kuwa ujenzi wa shule hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.

 Sauti ya mwalimu wa shule ya Kasokola inayojengwa katika kata ya Kasokola

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameomba radhi kwa kusuasua kwa mradi huo na kuahidi kusimamia kikamilifu mradi huo uweze kukamilika kwa wakati na katika ubora unaotakiwa.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko