Mpanda FM

Katavi:Mbunge jimbo la Nsimbo akabidhi gari ya wagonjwa Itenka

8 January 2025, 12:24 pm

Gari la wagonjwa lililokabidhiwa na Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe.picha na Rachel Ezekia

Amewataka  wauguzi   na wananchi kutumia gari hilo kwa kufuata kanuni sheria na miongozo ya serikali”

Na Rachel Ezekia-Katavi

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Itenka Kilichopo hlmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Akikabidhi gari hilo la wagonjwa  Anna Lupembe Amewataka  wauguzi   na wananchi kutumia gari hilo kwa kufuata kanuni sheria na miongozo ya serikali  na kusema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo kuboresha huduma ya nishati na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami .

Sauti ya mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe

Kwa upande wake Mbonimpaye Nkoronko  Akimuwakilisha  Mkuu wa wilaya Jamila Yusuph amewataka wananchi wa kata hiyo kutokiuka matumizi ya gari hilo la wagonjwa huku akisisistiza juu  ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu

Sauti ya Mbonimpaye Nkoronko  Akimuwakilisha  Mkuu wa wilaya Jamila Yusuph

Mbunge jimbo la Nsimbo aliyeketi kati ,huku kushoto ni mwakilishi wa mkuu wa wilaya Mbonimpaye Nkoronko  

Nao baadhi ya wananchi  wakizungumza baada ya makabidhiano hayo wameahidi kulitumia kwa mujibu wa sheria na kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa kipindupindu.

Sauti ya baadhi ya wananchi  wakizungumza baada ya makabidhiano hayo