Katavi:BoT yatoa elimu ya utunzaji wa sarafu kwa wenye ulemavu
24 December 2024, 1:03 pm
“wamenufaika na Elimu hiyo kwa kuzitambua alama za sarafu na usalama wake“
Na Edda Enock -Katavi
Benki kuu ya Tanzania imetoa Elimu ya utunzaji wa sarafu na kutambua alama za usalama kwenye sarafu kwa watu wenye changamoto ya kusikia [viziwi] mkoani Katavi.
Noves Moses meneja msaidizi idara ya mawasiliano benki kuu ya Tanzania amesema kuwa lengo la kuleta Elimu hiyo ni kuwawezesha kuwa salama wakati wanafanya shughuli zao za kiuchumi.
Sauti ya Noves Moses meneja msaidizi idara ya mawasiliano benki kuu ya Tanzania
Nao baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wenye changamoto ya kusikia wamesema kuwa wamenufaika na Elimu hiyo kwa kuzitambua alama za sarafu na usalama wake na kuiomba serikali kuendelea kutoa Elimu.
Sauti za baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo
Mafunzo hayo yametolewa nchi nzima ambayo yanalenga kutoa Elimu ya utunzaji bora wa sarafu kwa chama cha viziwi Tanzania (TAMAVITA).