Mpanda FM

RC Katavi awataka wazazi kuwapeleka shule watoto waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza

24 December 2024, 12:35 pm

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akiwa ofisini kwake.picha na Ben Gadau

wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu watajiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwakuwa tayari vyumba vya madarasa vimekamilika

Na Ben Gadau-Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka wanafunzi waliofaulu kujiunga na Elimu ya kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2025.

Ameyasema hayo wakati akizungumnza na waandishi wa habari wa mkoa wa katavi ofisini kwake.

Amesema kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu watajiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwakuwa tayari vyumba vya madarasa vimekamilika.

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Aidha Mwanamvua amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Katavi imejipanga kuhakikisha inamaliza changamoto ya madawati katika vyumba vya madarasa ili kuwapa nafasi wanafunzi hao kusoma na kupata ufaulu mzuri.

Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko

Mkuu wa Mkoa amewatakia Kheri ya sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya wananchi wote wa Mkoa wa Katavi na kuwataka kusherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.